Search This Blog

Monday, September 4, 2017

RUBANI WA NDEGE YA KIJESHI AANGUKA WAKATI WA MAONYESHO


Rubani wa kijeshi ameripotiwa kuanguka na kufa kutoka kwenye ndege ya helikopta aliyokuwa akiendesha zaidi ya mita 1,300 angani wakati ya maonyesho ya ndege za kijeshi nchini Ubelgiji.

Rubani huyo alikuwa akiendesha helikopta aina ya Agusta A-109 alipoanguka kutoka kwenye kiti chake. Rubani mwenzake aliyekuwa nay eye kwenye ndege hiyo alishika usukani na akaweza kuidhibiti ndege hiyo. Uchunguzi wa awali umebaini kwamba huenda rubani huyo aliruka kwa makusudi ili kujitoa uhai. Marubani hao wa kijeshi walikuwa wakionyesha ujuzi wao wa uendeshaji wa ndege wakati wa ajali hiyo. Uchunguzi zaidi umeanzishwa kuhusiana na tukio hilo.
Share: