Kiwanda cha silaha cha Degtyarev na Mfuko wa utafiti katika mustakabali wa Russia vimesanifu kwa pamoja roboti ya vita ya "Nerekhta-2".
Roboti hii inayofanana na kifaru kidogo ina urefu wa mita 2.5, upana wa mita 1.6 na kimo cha mita 0.9, na uzito wake ni tani 1 hivi.
Roboti hii inaweza kufanya doria, kuchunguza, kusaidia mapambano, kufanya mawasiliano, na kusafirisha watu na vitu. Ina bunduki moja nyepesi yenye kipenyo cha milimita 7.62 na bunduki moja nzito yenye kipenyo cha milimita 12.7. Watafiti pia wanapanga kuweka mzinga mdogo kwenye roboti hii.
Askari wanaweza kuwasiliana na roboti hii kwa remote kwa umbali wa kilomita 3. Pia inaweza kuendeshwa kwa maneno au ishara ya mikono. Askari akitaka roboti hii kumsaidia, anatakiwa kupunga silaha yake kwa njia maalum, baadaye roboti inafyatulia risasi kitu au mtu aliyelengwa.
Mchana roboti hii inaweza kutambua shabaha iliyoko umbali wa kilomita 5 kutoka mahali ilipo kwa darubini, na usiku inaweza kutambua shabaha iliyoko kilomita 4 kwa kifaa cha kuonea usiku.
Roboti hii ina injini yenye nguvu kubwa, na inaweza kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 32 kwa saa. Inapofanya kazi ya usafirishaji, inaweza kubeba vitu vyenye uzito wa kilo 700.
Askari mmoja anaweza kuziongoza roboti 18 kufanya kazi kwa pamoja kwa remote moja tu.
-
This density map of the cerebral cortex of a mouse shows which neurons get activated when the animal explores of a new environment. The l...
-
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema wakati umefika sasa wa kubadili mfumo kutoka ule wa kutege...
-
Rais Azali Assoumani wa Comoro amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na ...
-
Jeshi la Polisi limeibuka kinara miongoni mwa taasisi 91 za Serikali zilizolimbikiza madeni hadi kufikia Sh1.4 trilioni, ripoti ya Mdhibiti ...
-
Donald Trump ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Republican katika majimbo matano ya Marekani yaliyopiga kura Jumanne. Mgo...
-
UGANDA: Rais Museveni ametoa kauli ya mwisho kuwa Bomba la Mafuta litapita njia ya Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga. -Kauli hiyo...
-
Baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa Juliet Kairuki, mjadala umeibuka kuhusu kitendo cha mkurugenzi huyo mtendaji wa Kituo cha Uwe...
-
Mahakama kuu Afrika kusini imeruhusu kuangaliwa upya uamuzi uliopitishwa 2009 wa kutupilia mbalia mashtaka yote ya ufisadi dhidi ya rais Jac...
-
Yanga imeingia kambia nchini Uturuki kwa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo za makundi Zimebaki siku chache kabla ya mab...
-
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea ushauri uliotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) wa kuishit...
0 comments:
Post a Comment