Kulitokea kizaazaa mapema wiki hii jijini Nairobi baada ya jamaa mmoja kujipata kwenye njia panda. Jamaa huyu amekuwa na mpenzi wa Facebook ambaye aliamua wakutane kwenye mojawalo ya lodgings jijini.
Siku ya kukutana ilipofika, baba watoto akamhadaa mkewe kuwa ameenda biashara nje ya jiji na kuwa angerejea siku inayofuata. Asichojua mkewe ni kwamba, jamaa alikuwa anaenda kukutana na 'mpango wa kando'.
Nyumbani, jamaa ana watoto watatu, akiwemo binti wa chuo kikuu. Binti huyu vile vioe akawadanganya wazazi wake kuwa alikuwa anaenda safari ya shule na hivyo apewe ruhusa. Kumbe lengo la binti huyu ni kukutana na 'mwanaume' wake wa Facebook.
Hapa, baba mtu hajajua kuwa huyu binti yake ndiye 'mpango wake wa kando'. Kisa na maana-WAMEKUWA WAKITUMIA PICHA BANDIA KWENYE FACEBOOK NA VILE VILE HAWAJAWAHI KUPIGIANA SIMU. WAO HUTUMIANA JUMBE TU KWENYE FACEBOOK.
Haya basi , mume akaaga familia yake, akiwemo msichana 'mpango wa kando' ambaye alitarajiwa kusafiri jioni 'safari ya shule'.
Baada ya kufika kwenye lodging, baba mtu akamtumia mrembo ambaye kwenye 'picha' za Facebook, alikuwa ameumbwa akaumbika. Si kiuno, si makalio, si sura, si ngozi laini, si macho ya gololi, nakadhalika, ujumbe wa kumwelekeza kwenye chumba cha kulala.
Baba mtu akaitisha chakula ndani ya chumba huku akisubiri windo lake. Mzee wa wenyewe akaoga, kuhakikisha kuwa hanuki jasho. Akajipuliza manukato... Yote kwa matayarisho ya kumpokea 'mgeni'. Mzee alikuwa amemtumia ujumbe mrembo na kumwelekeza kulikokuwa chumba. Baada ya saa kadhaa za kusubiri kwa hamu na hamumu, mtoto wa wenyewe akawasili. Akaelekea moja kwa moja hadi kwenye chumba alichokuwa ameelekezwa na 'mchumba' wake.
Msichana akabisha mlango wa chumba. Baba mtu akajinyoosha, tayari kumlaki mgeni. Alipofungua mlango, amini usiamini alizirai. Mwanamke aliyekuwa akimtarajia ni binti yake. Aibu gani hii!!! #MapenziYaFacebook
0 comments:
Post a Comment