JPM ATENGUA UTEUZI WA MA-DC WATATU WAKATI WA KUAPISHWA
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya watatu huku mmoja akiwa amebakiza muda mfupi kabla ya kula kiapo cha uadilifu, Ikulu, Dar es Salaam.Imegundulika kuwa wawili waliteuliwa kimakosa na mmoja tayari ana wadhifa mwingine wa ubunge.Akitoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo Ikulu Dar es Salaam jana, wakati wa kuapisha wakuu wa mikoa wapya watatu na shughuli ya kula kiapo cha uadilifu kwa ma-DC wapya 139, Dk Magufuli alisema alitengua uteuzi wa Fikiri Avias Said kwa kuwa jina lake lilikosewa.Alisema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi mkoani Singida ni Miraji Mtaturu. Mtaturu alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza.
Aidha, Dk Magufuli alisema ametengua uteuzi wa Fatma Toufiq kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa kuwa tayari mteule huyo ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Badala yake, nafasi hiyo imezibwa na Agnes Hokororo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho tawala. Katika Serikali ya Awamu ya Nne, Toufiq alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.“Nilishasema katika utawala wangu, kila kazi itakuwa na mtu mmoja ili kuwe na ufanisi katika utendaji. Mtu mmoja, kazi moja,” alisisitiza Rais Magufuli akifafanua kuhusu Fatma Toufiq.
0 comments:
Post a Comment