Search This Blog

Wednesday, June 29, 2016

TANZANIA NA COMORO ZAAHIDIANA USHIRIKIANO SEKTA MBALIMBALI

Times Fm TZ's photo.

Rais Azali Assoumani wa Comoro amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na biashara.Alitoa kauli hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Umrah.Amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za kijamii na kusisitiza serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Comoro.
Akitoa ujumbe wa Rais Magufuli kwa Rais Assoumani, Makamu wa Rais Samia amemhakikishia rais huyo wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais Assoumani kheri katika safari yake ya Makka kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Share:

0 comments:

Post a Comment