Search This Blog

Wednesday, June 29, 2016

MAKONDA AVUTANA NA HALMASHAURI KUHUSU KAMPUNI ZA UJENZI



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Dar es Salaam. Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizuia Kampuni ya Ujenzi ya Delmont kupewa zabuni upya jijini hapa hadi atakapojiridhisha, Kamati ya Fedha ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, imeiruhusu kumalizia kazi iliyoianza.
Juni 24, Makonda alisitisha utoaji upya wa zabuni kwa kampuni nne za makandarasi ikiwamo ya Delmont, kwa kile alichodai zina uwezo mdogo wa ujenzi.
Kamati hiyo ikiongozwa na Meya wa manispaa hiyo, Boniface Jacob ilitoa uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kukagua barabara ya Mabatini hadi Kijitonyama inayodaiwa kujengwa chini ya kiwango na kampuni hiyo.
Mhandisi wa Delmont, Salutari Mushi alisisitiza kuwa hawana makosa na wanafanya kile walichoelekezwa na wahandisi kupitia mwongozo na michoro ya usanifu.
Share:

0 comments:

Post a Comment