Dodoma. Wabunge wa Ukawa wamemtaka Rais John Magufuli kutoa tamko juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar na kwamba, wana mpango wa kumpeleka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakidai yanayotokea visiwani humo yana baraka zake.
Katika mkutano wao na wanahabari jana, wabunge hao wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwenda Zanzibar kujionea hali halisi badala ya kupata taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.
Hata hivyo, CCM imesema inalaani tamko hilo na kuwa kama Ukawa wanaona kuna masuala yanayohitaji kurekebishwa na kuhitaji hatua za haraka za Serikali watumie vyombo vinavyotambulika kisheria kama Bunge badala ya kuishia kulalamika “vichochoroni”.
Akitoa tamko la wabunge hao jana, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alieleza kuwa hali ya kiusalama inazidi kuwa mbaya Pemba na Unguja baada ya uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kutokana na baadhi ya wananchi kupigwa na vikosi alivyodai ni vya usalama.
0 comments:
Post a Comment