Kigoma. Baada ya kuteseka muda mrefu, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) inatarajia kuanza ujenzi wa madaraja manne yakatayounganisha barabara kuu ya Mahale hadi mji wa Kigoma.
Hivi sasa watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mahale wanalazimika kusafiri kwa siku mbili majini kutoka Kigoma Mjini, huku wananchi wakitumia muda huohuo kutoka Mahale hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Uvinza yaliyopo mjini Kigoma.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi wa maeneo hayo hawawezi kwenda mjini na wakiamua kwenda inawalazimu kupanda boti Ziwa Tanganyika na kusafiri kwa siku hizo kutokana na ukosefu wa barabara, suala linalosababisha wakose fursa nyingi za uchumi.
Madaraja hayo yanajengwa kwenye kipande cha barabara chenye urefu wa kilomita 38 katika kata za Buhingu, Kalyia na Igalula wilayani Uvinza kwa gharama ya Sh1.84 bilioni.
0 comments:
Post a Comment