Yanga imeingia kambia nchini Uturuki kwa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo za makundi
Zimebaki siku chache kabla ya mabingwa wa Tanzania bara Yanga kutupa karata ya kwanza kwenye kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, Yanga imeingia kambia nchini Uturuki kwa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo za makundi, na tayari benchi la ufundi limeanza boresha timu kwa kuongeza wachezaji kama Kessy, Vicent Adrew, Juma Mahadhi na Ben Kakolanya
Goal inakuchambulia wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya makundi shirikisho Afrika
Tp Mazembe
Timu kutoka Congo imeanzishwa mwaka 1939, ni mabingwa mara tano wa klabu bingwa Afrika , timu inayo milikiwa na tajiri wa madini nchini Congo Moise Katumbi Tp Mazembe wanatumia uwanja wao wa Stade duTp Mazembe unachukua watazamaji 18500, vijana wa kocha Hubert Velud wanaongoza ligi kuu nchini mwao baada ya michezo 9 wamejikusanyia pointi 23 tatu zaidi ya timu inayowafuatia. Wamekusanya wachezaji wazoefu kwenye michuano hii kama Kidiaba, Singuluma na Kasusula. Mtu ambaye ni tegemezi kwenye timu hii Adama Traore raia wa Mali na Roger Assale raia wa Ivory Coast.
Mo Bejaia
Timu kutoka Algeria imeanzishwa mnamo mwaka 1954, si timu maarufu Afrika na hata nchini mwao hawana historia kubwa zaidi ya kuchukua ubingwa wa Fa 2015 wanatumia uwanja wa Stade I’unite Maghrebine uliopo mji wa Bejaia unachukua watazamaji 19000 tu, wako nafasi ya sita kwenye ligi yao baada ya michezo 30 wamejikusanyia alama 44. Wachezaji wao hatari ni Mouhamed Ndoye raia wa Senegal anayecheza kiungo cha kushambulia na Zahir Zerdab.
Medeama Sc
Kwenye kundi hili hii ndiyo timu changa kuliko zote imeanzishwa mwaka 2002 nchini Ghana katika mji wa Tarkwa, uwanja wao wa nyumbani wa Tarkwa T & A Park unachukua watazamaji 5000 na ni timu pekee inayonolewa na mzawa katika kundi hili Bw. Prince Owusu raia wa Ghana, wanashika nafasi ya tano kwenye timu 16 ligi kuu ya Ghana baada ya kujikusanyia alama 26 kwenye michezo 15 pointi mbili zaidi na anaeongoza ligi nchini mwao. Si timu kubwa kwenye ukanda huu wa Afrika na haina historia yeyote kwenye michuano hii, kikubwa wanacho jivunia ni ubingwa wa Super Cup walio upata mwanzoni wa mwaka huu. Mtu ambaye ambaye yupo nyuma ya mafanikia yao ni kiungo Kwesi Donsu na mshambuliaji mdogo Bismack Oppong.
0 comments:
Post a Comment