Search This Blog
Monday, September 4, 2017
Tuesday, August 9, 2016
KUTANA NA HISTORIA YA MWIZI WA BENKI ALIYESUMBUA MIAKA 30 BILA KUKAMATWA
Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..
Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..
Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..
Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..
WARAKA MZITO WA LEMA KWA JPM
Mh Rais nakusalimu, sasa ni usiku wa manane nimeamka nikiwa natafakari mambo mengi lakini zaidi sana ni kuhusu mwenendo wa demokrasia katika Nchi yetu, nimekosa usingizi kabisa nikifikiri ni namna gani ninaweza kusaidia kwa mawazo yangu kufanikisha nia yako njema katika ustawi wa Nchi yetu.
Mheshimiwa Rais na kabla sijaanza kuandika waraka huu kwako, nimesali nipate hekima ya kutosha juu ya maandishi haya ninayoandika na wewe pia nimekuombea sana kwa Mungu, kwani baada ya mimi na Wabunge wenzangu kufukuzwa Bungeni kwa kudai matangazo ya Bunge live nilikwenda kijijini kwetu kusalimia wazazi wangu, na nilipokuwa nawaelezea kwanini nimefukuzwa Bungeni matamshi yangu yalikuwa na laumu nyingi dhidi ya Serikali yako, Mama yangu aliniuliza kama huwa nakuombea kwa Mungu kama Rais wa Nchi, sikuwa na jibu la uaminifu kwake na hivi ndivyo alivyoniambia “ KAZI YA URAIS NI NGUMU, KILA MARA UNAPOSALI USIACHE KUMWOMBEA RAIS WA NCHI, MUNGU AMAJILIE AFYA NJEMA, HEKIMA NA BUSARA KWANI RAIS AKIKOSEA KUAMUA NI NCHI IMEKOSEA SAFARI YAKE YA MAFANIKIO NA USTAWI, KWA HIYO MUOMBEE RAIS SIKU ZOTE “
Mheshimiwa Rais, ulikuwa ni husia muhimu sana kwangu lakini mgumu sana kwa wakati huo, lakini baada ya kutafakari, kuanzia siku hiyo mimi na Familia yangu tumekuwa tukikuombea sana kwa Mwenyezi Mungu ili Nchi yetu isikosee safari yake ya mafanikio yaliyojaa Ustawi bora na Uhuru.
Mheshimiwa Rais, kama ambavyo naamini Watu wengi wanakuombea na Sisi pia tunaomba utuombee, Mungu atujalie hekima, busara na uvumulivu juu ya maumivu tunayopitia wakati tunapojaribu kutekeleza wajibu wetu wa kidemokrasia katika Nchi yenye msingi wa demokrasia lakini kwa bahati mbaya sana kazi zetu za siasa zimekuwa ngumu sana na mashaka kuliko hata wakati ule wa ukoloni.
Mheshimiwa Rais, Ukimchukua ndege porini ukamfuga nyumbani ,ukamtengenezea kiota cha pamba na sufi, ukampa chakula chake kwa ufasaha na asikose maji ya kunywa tena masafi ya chupa ya Kilimanjaro, ukamfungia ndani asipate tabu juani, hakika siku ukiacha mlango au dirisha wazi ataondoka na hatarudi, atakwenda porini akatafute asili yake na Uhuru wake, atakwenda kutafuta chakula kwa shida, maji kwa shida, lakini lengo muhimu ambalo ni Uhuru litampa faraja kubwa ya kwamba ameondoka kizuizini.
Mheshimiwa Rais, unaweza ukatupa chakula, elimu, afya, na mambo mengi muhimu, lakini ukitunyima Uhuru wa kusema, tukaishi kwa hofu kama tuliyonayo sasa, Mheshimiwa Rais nakuhakikishia siku ukiacha dirisha wazi tutatoroka na kamwe hatutarudi. Aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muhamar Gaddafi, alifanya kazi kubwa ya kujenga Libya hata mahari watu walilipiwa na Serikali walipotaka kuoa, watu walipewa nyumba na mambo mengi muhimu, lakini Gaddafi alisahau kuwa hakuna zawadi kubwa kwa Binadamu zaidi ya Uhuru.
Mheshimiwa Rais, ruhusu Watu waseme, acha Watu wapige kelele, ruhusu mioyo yao ipumue, wacha Watu wakosoe jambo hili halitakuwa balaa kwako bali Baraka. Kama kweli unayo nia njema, njia pekee na muhimu tu unayoweza kuthibitisha nayo nia yako njema ni kuruhusu mfumo wa demokrasia wa Vyama vingi kukua, umekuwa ukipigana sana na mambo mengi machafu yaliofanywa na Serikali ya Chama chako huko nyuma, umethibitisha kwetu kwa kiwango fulani na kwa umma wote hali mbaya uliyoikuta Serikalini baada ya kuingia Ikulu, hili funzo tosha kwako kwamba namna pekee ya kusaidia Taifa hili ni kujenga demokrasia ya dhati na kufufua matumaini ya Watanzania kwa kuwapa Katiba bora waliyoitaka, ambayo hata kama uwepo wako hautakuwepo Watanzania watakuwa salama na watasonga mbele.
Mheshimiwa Rais, mamlaka uliyonayo yanatokana na Katiba , Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Nchi kwa sababu ya Katiba, Majeshi yote yanakutii wewe ni kwa sababu ya Katiba, uteuzi wote unaofanya wa Viongozi katika utawala na unaowatumbua, mamlaka hayo pia umepewa na Katiba, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pia ni matakwa ya Katiba na tumepewa na Katiba ,na wote sisi kwa dini zetu mbali mbali na makabila yetu wote tunakutana na kuunganishwa na Katiba na kuheshimu Katiba kama msingi mkuu wa uendeshaji wa Nchi.
Mheshimiwa Rais, Mungu adhihakiwi kwani apandacho Mtu ndicho avunacho,Wazazi wengi wanalia sana siku hizi juu ya tabia ya kwamba watoto wao wamekuwa walevi na wenye adabu mbaya, lakini ukifanya utafiti karibu nyumba zote za kisasa zinazojengwa siku hizi ramani ya nyumba hizo hazikosi baa ndogo ndani ya nyumba hizo, kama hatuwezi kufanya tunayo ruhusiwa na Katiba na anayetuzuia kufanya hivyo mamlaka yake yanatokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa hapa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, iko siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu Katiba na utawala wa sheria hautakuwepo.
Mheshimiwa Rais, Haki huinua Taifa,tuanapoelekea tarehe 1/09/2016, CHADEMA imeitisha mikutano ya hadhara kote Nchini pamoja na maandamano, tayari kauli yako na viongozi wengine wa juu wa Serikali wameonya juu ya Mikutano hiyo na kusema hatua kali zitachukuliwa bila huruma dhidi ya watu wote watakaojitokeza kuunga mkono harakati hizo.
Mheshimiwa Rais, tunafahamu Jeshi la Polisi liko imara kupambana na kuzuia haki hii ya Kikatiba, pengine Watu wataumia na wengine watakufa, je ni kweli tunahitaji kufika huko? je hatuoni kuwa matakwa ya Katiba yakizingatiwa risasi wala bomu havitatumika, maandamano haya yameitishwa kushinikiza haki yetu ya Kikatiba ya kufanya mikutano, Uhuru huu wa Katiba ukizingatiwa kwa kuruhusu mikutano ya hadhara hakika ni kwamba maandamano hayatakuwepo na kusema kwamba Sasa ni Kazi tu, na mikutano yote ya Siasa isubiri 2020, je ni halali Mkristo kusali siku ya Noeli (Christmas ) tu ? au Mwislamu kuingia Msikitini siku ya Idd tu?
Mheshimiwa Rais, Siasa ni Kazi na ndio maana wewe ni Rais kwa sababu ya Siasa na Mimi ni Mbunge kwa sababu ya Siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbali mbali na wa juu kabisa katika Nchi.
Mheshimiwa Rais, lakini pia kufuatia kauli yako ya kwamba kila Mtu afanye mkutano kule alikochaguliwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa letu na mshikamano kwani tunajenga siasa za ukanda na ukabila katika Nchi yetu. Mkoa wa Kilimanjaro ccm ina majimbo mawili tu, maana yake CCM hawatakiwi kufanya mikutano ya hadhara na siasa sehemu nyingine za Mkoa wa Kilimanjaro? Mkoa wa Geita hauna hata Jimbo moja la Upinzani, je huko nako vyama vyetu havitakiwi kwenda kufanya mikutano na ujenzi wa chama? Je, ikiendelea hivi huoni kuwa tutaanza kujenga misingi ya kugombania nafasi za siasa kule ambako ni asili za makabila yetu tu?
Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika Taifa letu ni kauli inayopaswa kerekebishwa haraka , hivi Karibuni Msemaji wa ccm Ole Sendeka alifanya Mkutano Longido, je Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? au Polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lako?
Mheshimiwa Rais, nakuomba sana utambue kwamba, unyenyekevu sio utumwa wala uzembe, ukizingatia matakwa ya Katiba hakuna mwenye hekima hatakaye kudharau, wewe ni Binadamu unaweza ukufanya makosa usiruhusu mikono yako ikashika damu pasipo sababu ya msingi ni laana kwa Taifa na Kizazi chako.
Mheshimiwa Rais, na kama jambo hili ambalo liko wazi katika Katiba yetu halitaweza kupata fikra yako na mwelekeo mpya wa mawazo yako, basi itakuwa ni dhahiri kwamba unachokitafuta katika utawala wako sio haki ya Watanzania bali ni utukufu binafsi. Na suala lolote kuhusu utukufu ni suala linalomuhusu Mungu na sio Binadamu
Mheshimiwa Rais, Polisi wanajiandaa kwa sababu ni muhimu wakatii amri ya Amiri Jeshi Mkuu, wasipofanya hivyo watakuwa wanafanya uhaini, lakini ni vyema ikajulikana kwamba, dhamira ikichoka huwa inatamani mauti, tukikaa kimya huku dhamira zetu zikiumia ni hatari kuliko kupiga kelele kwa sauti kuu, ni maombi yangu kwa Mungu kwamba muufaka wa utata huu wa Uhuru wa Vyama vya Siasa unaotokana na Katiba uwe umepatikana mapema iwezekanavyo ili kuepusha hatari inayoweza kutokea na kusabibisha maumivu , hasara, vifo na utengano katika Taifa letu.
Mheshimiwa Rais, wakati Polisi wanajiandaa kukabiliana na waandamanaji wanaodai haki yao ya kweli, chuki kubwa inaendelea kujengwa kati ya walinzi hawa wa amani na raia, mashaka yangu ni kwamba kunaweza kutatokea mpasuko mkubwa huko mbele ya safari kati ya Polisi na raia, maisha ya visasi yataanza mitaani na mwelekeo mbaya wa Taifa letu unaweza kutokea.
Mwisho, Mheshimiwa Rais, nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki sana katika kazi zako na maamuzi yako ya kila siku , ila siku zote kumbuka" Haki huinua Taifa"
“Never forget that justice is what love looks like in public“ Cornel West
“injustice anywhere is a threat to justice everywhere” Martin Luther JR“
“Peace and justice are two sides of the same coin“ Dwight D.Eisenhower
“All the great things are simple , and many can be expressed in a single word, freedom , justice, honor, duty, mercy, hope” Winston Churchill
Godbless J Lema (MB)
Monday, August 8, 2016
RUSSIA YAZINDUA ROBOTI YENYE UMBO LA KIFARU
Kiwanda cha silaha cha Degtyarev na Mfuko wa utafiti katika mustakabali wa Russia vimesanifu kwa pamoja roboti ya vita ya "Nerekhta-2".
Roboti hii inayofanana na kifaru kidogo ina urefu wa mita 2.5, upana wa mita 1.6 na kimo cha mita 0.9, na uzito wake ni tani 1 hivi.
Roboti hii inaweza kufanya doria, kuchunguza, kusaidia mapambano, kufanya mawasiliano, na kusafirisha watu na vitu. Ina bunduki moja nyepesi yenye kipenyo cha milimita 7.62 na bunduki moja nzito yenye kipenyo cha milimita 12.7. Watafiti pia wanapanga kuweka mzinga mdogo kwenye roboti hii.
Askari wanaweza kuwasiliana na roboti hii kwa remote kwa umbali wa kilomita 3. Pia inaweza kuendeshwa kwa maneno au ishara ya mikono. Askari akitaka roboti hii kumsaidia, anatakiwa kupunga silaha yake kwa njia maalum, baadaye roboti inafyatulia risasi kitu au mtu aliyelengwa.
Mchana roboti hii inaweza kutambua shabaha iliyoko umbali wa kilomita 5 kutoka mahali ilipo kwa darubini, na usiku inaweza kutambua shabaha iliyoko kilomita 4 kwa kifaa cha kuonea usiku.
Roboti hii ina injini yenye nguvu kubwa, na inaweza kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 32 kwa saa. Inapofanya kazi ya usafirishaji, inaweza kubeba vitu vyenye uzito wa kilo 700.
Askari mmoja anaweza kuziongoza roboti 18 kufanya kazi kwa pamoja kwa remote moja tu.
Saturday, July 2, 2016
MWANAUME AZIRAI BAADA YA KUKUTANA NA MCHEPUKO WAKE FACEBOOK AMBAYE NI MWANAE
Kulitokea kizaazaa mapema wiki hii jijini Nairobi baada ya jamaa mmoja kujipata kwenye njia panda. Jamaa huyu amekuwa na mpenzi wa Facebook ambaye aliamua wakutane kwenye mojawalo ya lodgings jijini.
Siku ya kukutana ilipofika, baba watoto akamhadaa mkewe kuwa ameenda biashara nje ya jiji na kuwa angerejea siku inayofuata. Asichojua mkewe ni kwamba, jamaa alikuwa anaenda kukutana na 'mpango wa kando'.
Nyumbani, jamaa ana watoto watatu, akiwemo binti wa chuo kikuu. Binti huyu vile vioe akawadanganya wazazi wake kuwa alikuwa anaenda safari ya shule na hivyo apewe ruhusa. Kumbe lengo la binti huyu ni kukutana na 'mwanaume' wake wa Facebook.
Hapa, baba mtu hajajua kuwa huyu binti yake ndiye 'mpango wake wa kando'. Kisa na maana-WAMEKUWA WAKITUMIA PICHA BANDIA KWENYE FACEBOOK NA VILE VILE HAWAJAWAHI KUPIGIANA SIMU. WAO HUTUMIANA JUMBE TU KWENYE FACEBOOK.
Haya basi , mume akaaga familia yake, akiwemo msichana 'mpango wa kando' ambaye alitarajiwa kusafiri jioni 'safari ya shule'.
Baada ya kufika kwenye lodging, baba mtu akamtumia mrembo ambaye kwenye 'picha' za Facebook, alikuwa ameumbwa akaumbika. Si kiuno, si makalio, si sura, si ngozi laini, si macho ya gololi, nakadhalika, ujumbe wa kumwelekeza kwenye chumba cha kulala.
Baba mtu akaitisha chakula ndani ya chumba huku akisubiri windo lake. Mzee wa wenyewe akaoga, kuhakikisha kuwa hanuki jasho. Akajipuliza manukato... Yote kwa matayarisho ya kumpokea 'mgeni'. Mzee alikuwa amemtumia ujumbe mrembo na kumwelekeza kulikokuwa chumba. Baada ya saa kadhaa za kusubiri kwa hamu na hamumu, mtoto wa wenyewe akawasili. Akaelekea moja kwa moja hadi kwenye chumba alichokuwa ameelekezwa na 'mchumba' wake.
Msichana akabisha mlango wa chumba. Baba mtu akajinyoosha, tayari kumlaki mgeni. Alipofungua mlango, amini usiamini alizirai. Mwanamke aliyekuwa akimtarajia ni binti yake. Aibu gani hii!!! #MapenziYaFacebook
Thursday, June 30, 2016
JPM ATENGUA UTEUZI WA MA-DC WATATU WAKATI WA KUAPISHWA
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya watatu huku mmoja akiwa amebakiza muda mfupi kabla ya kula kiapo cha uadilifu, Ikulu, Dar es Salaam.Imegundulika kuwa wawili waliteuliwa kimakosa na mmoja tayari ana wadhifa mwingine wa ubunge.Akitoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo Ikulu Dar es Salaam jana, wakati wa kuapisha wakuu wa mikoa wapya watatu na shughuli ya kula kiapo cha uadilifu kwa ma-DC wapya 139, Dk Magufuli alisema alitengua uteuzi wa Fikiri Avias Said kwa kuwa jina lake lilikosewa.Alisema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi mkoani Singida ni Miraji Mtaturu. Mtaturu alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza.
Aidha, Dk Magufuli alisema ametengua uteuzi wa Fatma Toufiq kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa kuwa tayari mteule huyo ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Badala yake, nafasi hiyo imezibwa na Agnes Hokororo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho tawala. Katika Serikali ya Awamu ya Nne, Toufiq alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.“Nilishasema katika utawala wangu, kila kazi itakuwa na mtu mmoja ili kuwe na ufanisi katika utendaji. Mtu mmoja, kazi moja,” alisisitiza Rais Magufuli akifafanua kuhusu Fatma Toufiq.
KUTANA NA TEKNOLOJIA YA KUCHAJI SIMU 8 BILA WAYA
Teknolojia ya kuchaji bila waya bado haitumiki sana, kwa sababu kuchaji kwa njia hii kunahitaji muda, tena vyombo vichache tu vya elektroniki vinatumia teknolojia hii. Hivi karibuni kampuni moja imetangaza chombo kipya cha kuchaji bila waya kiitwacho "Fli Charge". Kinaweza kuchaji simu yako kwa kasi na ufanisi mkubwa, hata huna haja ya kuweka simu yako kwenye ubao wa kuchaji. Kampuni hiyo pia imetengeneza plagi maalum kwa microUSB na kwa simu za IPhone, hivyo simu za kawaida aina ya smartphone pia zinaweza kuchajiwa na chombo hiki kwa kuunganishwa na plagi hizi, Chombo hiki kinatoa Watt 40 za umeme, kinaweza kuchaji simu 8 kwa wakati mmoja. Hii ni habari nzuri kwa watu wenye simu nyingi. Lakini ukichaji simu nyingi zaidi kwa wakati mmoja, ufanisi wake unapungua. Hivi sasa kampuni yake inakusanya uwekezaji kwenye tovuti ya Indiegogo, inapanga kukusanya dola za kimarekani laki moja ili kuzalisha chombo hiki. Lengo hili likitimizwa, chombo hiki kinatazamiwa kuanza kuuzwa mwezi Oktoba mwaka huu. CRI Kiswahili's photo.