Search This Blog

Tuesday, August 9, 2016

KUTANA NA HISTORIA YA MWIZI WA BENKI ALIYESUMBUA MIAKA 30 BILA KUKAMATWA

MUHALIFU WA BENKI MWENYE AKILI KULIKO WOTE (THE MOST PROLIFIC BANK ROBBER)..
(Taarifa ya Kusisimua).
Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.
Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!
Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.
Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu
ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"
Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.
Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha..
Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)
Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.
Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)
Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza' sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank robber'..
#1
MAANDALIZI KABLA YA TUKIO
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..
Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake..
Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta, haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!
Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!
Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller, nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma personality zao..
Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..
Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe..
#2
UTEKELEZAJI WA TUKIO
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..
Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!
Now; siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa.. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi???
#3
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..
Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..
Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..
Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani..
Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'... Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata..
#4
KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno!
Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.
FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"
Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..
Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini na naamini kabisa Hollywood wanaomba usiku na mchana atoke salama ili wamfanye celebrity na watupe bonge la muvi.!!
Share:

WARAKA MZITO WA LEMA KWA JPM

Mh Rais nakusalimu, sasa ni usiku wa manane nimeamka nikiwa natafakari mambo mengi lakini zaidi sana ni kuhusu mwenendo wa demokrasia katika Nchi yetu, nimekosa usingizi kabisa nikifikiri ni namna gani ninaweza kusaidia kwa mawazo yangu kufanikisha nia yako njema katika ustawi wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Rais na kabla sijaanza kuandika waraka huu kwako, nimesali nipate hekima ya kutosha juu ya maandishi haya ninayoandika na wewe pia nimekuombea sana kwa Mungu, kwani baada ya mimi na Wabunge wenzangu kufukuzwa Bungeni kwa kudai matangazo ya Bunge live nilikwenda kijijini kwetu kusalimia wazazi wangu, na nilipokuwa nawaelezea kwanini nimefukuzwa Bungeni matamshi yangu yalikuwa na laumu nyingi dhidi ya Serikali yako, Mama yangu aliniuliza kama huwa nakuombea kwa Mungu kama Rais wa Nchi, sikuwa na jibu la uaminifu kwake na hivi ndivyo alivyoniambia “ KAZI YA URAIS NI NGUMU, KILA MARA UNAPOSALI USIACHE KUMWOMBEA RAIS WA NCHI, MUNGU AMAJILIE AFYA NJEMA, HEKIMA NA BUSARA KWANI RAIS AKIKOSEA KUAMUA NI NCHI IMEKOSEA SAFARI YAKE YA MAFANIKIO NA USTAWI, KWA HIYO MUOMBEE RAIS SIKU ZOTE “

Mheshimiwa Rais, ulikuwa ni husia muhimu sana kwangu lakini mgumu sana kwa wakati huo, lakini baada ya kutafakari, kuanzia siku hiyo mimi na Familia yangu tumekuwa tukikuombea sana kwa Mwenyezi Mungu ili Nchi yetu isikosee safari yake ya mafanikio yaliyojaa Ustawi bora na Uhuru.

Mheshimiwa Rais, kama ambavyo naamini Watu wengi wanakuombea na Sisi pia tunaomba utuombee, Mungu atujalie hekima, busara na uvumulivu juu ya maumivu tunayopitia wakati tunapojaribu kutekeleza wajibu wetu wa kidemokrasia katika Nchi yenye msingi wa demokrasia lakini kwa bahati mbaya sana kazi zetu za siasa zimekuwa ngumu sana na mashaka kuliko hata wakati ule wa ukoloni.

Mheshimiwa Rais, Ukimchukua ndege porini ukamfuga nyumbani ,ukamtengenezea kiota cha pamba na sufi, ukampa chakula chake kwa ufasaha na asikose maji ya kunywa tena masafi ya chupa ya Kilimanjaro, ukamfungia ndani asipate tabu juani, hakika siku ukiacha mlango au dirisha wazi ataondoka na hatarudi, atakwenda porini akatafute asili yake na Uhuru wake, atakwenda kutafuta chakula kwa shida, maji kwa shida, lakini lengo muhimu ambalo ni Uhuru litampa faraja kubwa ya kwamba ameondoka kizuizini.

Mheshimiwa Rais, unaweza ukatupa chakula, elimu, afya, na mambo mengi muhimu, lakini ukitunyima Uhuru wa kusema, tukaishi kwa hofu kama tuliyonayo sasa, Mheshimiwa Rais nakuhakikishia siku ukiacha dirisha wazi tutatoroka na kamwe hatutarudi. Aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muhamar Gaddafi, alifanya kazi kubwa ya kujenga Libya hata mahari watu walilipiwa na Serikali walipotaka kuoa, watu walipewa nyumba na mambo mengi muhimu, lakini Gaddafi alisahau kuwa hakuna zawadi kubwa kwa Binadamu zaidi ya Uhuru.

Mheshimiwa Rais, ruhusu Watu waseme, acha Watu wapige kelele, ruhusu mioyo yao ipumue, wacha Watu wakosoe jambo hili halitakuwa balaa kwako bali Baraka. Kama kweli unayo nia njema, njia pekee na muhimu tu unayoweza kuthibitisha nayo nia yako njema ni kuruhusu mfumo wa demokrasia wa Vyama vingi kukua, umekuwa ukipigana sana na mambo mengi machafu yaliofanywa na Serikali ya Chama chako huko nyuma, umethibitisha kwetu kwa kiwango fulani na kwa umma wote hali mbaya uliyoikuta Serikalini baada ya kuingia Ikulu, hili funzo tosha kwako kwamba namna pekee ya kusaidia Taifa hili ni kujenga demokrasia ya dhati na kufufua matumaini ya Watanzania kwa kuwapa Katiba bora waliyoitaka, ambayo hata kama uwepo wako hautakuwepo Watanzania watakuwa salama na watasonga mbele.

Mheshimiwa Rais, mamlaka uliyonayo yanatokana na Katiba , Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Nchi kwa sababu ya Katiba, Majeshi yote yanakutii wewe ni kwa sababu ya Katiba, uteuzi wote unaofanya wa Viongozi katika utawala na unaowatumbua, mamlaka hayo pia umepewa na Katiba, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pia ni matakwa ya Katiba na tumepewa na Katiba ,na wote sisi kwa dini zetu mbali mbali na makabila yetu wote tunakutana na kuunganishwa na Katiba na kuheshimu Katiba kama msingi mkuu wa uendeshaji wa Nchi.

Mheshimiwa Rais, Mungu adhihakiwi kwani apandacho Mtu ndicho avunacho,Wazazi wengi wanalia sana siku hizi juu ya tabia ya kwamba watoto wao wamekuwa walevi na wenye adabu mbaya, lakini ukifanya utafiti karibu nyumba zote za kisasa zinazojengwa siku hizi ramani ya nyumba hizo hazikosi baa ndogo ndani ya nyumba hizo, kama hatuwezi kufanya tunayo ruhusiwa na Katiba na anayetuzuia kufanya hivyo mamlaka yake yanatokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa hapa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, iko siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu Katiba na utawala wa sheria hautakuwepo.

Mheshimiwa Rais, Haki huinua Taifa,tuanapoelekea tarehe 1/09/2016, CHADEMA imeitisha mikutano ya hadhara kote Nchini pamoja na maandamano, tayari kauli yako na viongozi wengine wa juu wa Serikali wameonya juu ya Mikutano hiyo na kusema hatua kali zitachukuliwa bila huruma dhidi ya watu wote watakaojitokeza kuunga mkono harakati hizo.

Mheshimiwa Rais, tunafahamu Jeshi la Polisi liko imara kupambana na kuzuia haki hii ya Kikatiba, pengine Watu wataumia na wengine watakufa, je ni kweli tunahitaji kufika huko? je hatuoni kuwa matakwa ya Katiba yakizingatiwa risasi wala bomu havitatumika, maandamano haya yameitishwa kushinikiza haki yetu ya Kikatiba ya kufanya mikutano, Uhuru huu wa Katiba ukizingatiwa kwa kuruhusu mikutano ya hadhara hakika ni kwamba maandamano hayatakuwepo na kusema kwamba Sasa ni Kazi tu, na mikutano yote ya Siasa isubiri 2020, je ni halali Mkristo kusali siku ya Noeli (Christmas ) tu ? au Mwislamu kuingia Msikitini siku ya Idd tu?

Mheshimiwa Rais, Siasa ni Kazi na ndio maana wewe ni Rais kwa sababu ya Siasa na Mimi ni Mbunge kwa sababu ya Siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbali mbali na wa juu kabisa katika Nchi.

Mheshimiwa Rais, lakini pia kufuatia kauli yako ya kwamba kila Mtu afanye mkutano kule alikochaguliwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa letu na mshikamano kwani tunajenga siasa za ukanda na ukabila katika Nchi yetu. Mkoa wa Kilimanjaro ccm ina majimbo mawili tu, maana yake CCM hawatakiwi kufanya mikutano ya hadhara na siasa sehemu nyingine za Mkoa wa Kilimanjaro? Mkoa wa Geita hauna hata Jimbo moja la Upinzani, je huko nako vyama vyetu havitakiwi kwenda kufanya mikutano na ujenzi wa chama? Je, ikiendelea hivi huoni kuwa tutaanza kujenga misingi ya kugombania nafasi za siasa kule ambako ni asili za makabila yetu tu?

Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika Taifa letu ni kauli inayopaswa kerekebishwa haraka , hivi Karibuni Msemaji wa ccm Ole Sendeka alifanya Mkutano Longido, je Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? au Polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lako?

Mheshimiwa Rais, nakuomba sana utambue kwamba, unyenyekevu sio utumwa wala uzembe, ukizingatia matakwa ya Katiba hakuna mwenye hekima hatakaye kudharau, wewe ni Binadamu unaweza ukufanya makosa usiruhusu mikono yako ikashika damu pasipo sababu ya msingi ni laana kwa Taifa na Kizazi chako.

Mheshimiwa Rais, na kama jambo hili ambalo liko wazi katika Katiba yetu halitaweza kupata fikra yako na mwelekeo mpya wa mawazo yako, basi itakuwa ni dhahiri kwamba unachokitafuta katika utawala wako sio haki ya Watanzania bali ni utukufu binafsi. Na suala lolote kuhusu utukufu ni suala linalomuhusu Mungu na sio Binadamu

Mheshimiwa Rais, Polisi wanajiandaa kwa sababu ni muhimu wakatii amri ya Amiri Jeshi Mkuu, wasipofanya hivyo watakuwa wanafanya uhaini, lakini ni vyema ikajulikana kwamba, dhamira ikichoka huwa inatamani mauti, tukikaa kimya huku dhamira zetu zikiumia ni hatari kuliko kupiga kelele kwa sauti kuu, ni maombi yangu kwa Mungu kwamba muufaka wa utata huu wa Uhuru wa Vyama vya Siasa unaotokana na Katiba uwe umepatikana mapema iwezekanavyo ili kuepusha hatari inayoweza kutokea na kusabibisha maumivu , hasara, vifo na utengano katika Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, wakati Polisi wanajiandaa kukabiliana na waandamanaji wanaodai haki yao ya kweli, chuki kubwa inaendelea kujengwa kati ya walinzi hawa wa amani na raia, mashaka yangu ni kwamba kunaweza kutatokea mpasuko mkubwa huko mbele ya safari kati ya Polisi na raia, maisha ya visasi yataanza mitaani na mwelekeo mbaya wa Taifa letu unaweza kutokea.

Mwisho, Mheshimiwa Rais, nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki sana katika kazi zako na maamuzi yako ya kila siku , ila siku zote kumbuka" Haki huinua Taifa"

“Never forget that justice is what love looks like in public“ Cornel West

“injustice anywhere is a threat to justice everywhere” Martin Luther JR“

“Peace and justice are two sides of the same coin“ Dwight D.Eisenhower

“All the great things are simple , and many can be expressed in a single word, freedom , justice, honor, duty, mercy, hope” Winston Churchill

Godbless J Lema (MB)

Share:

Monday, August 8, 2016

RUSSIA YAZINDUA ROBOTI YENYE UMBO LA KIFARU

Kiwanda cha silaha cha Degtyarev na Mfuko wa utafiti katika mustakabali wa Russia vimesanifu kwa pamoja roboti ya vita ya "Nerekhta-2".
Roboti hii inayofanana na kifaru kidogo ina urefu wa mita 2.5, upana wa mita 1.6 na kimo cha mita 0.9, na uzito wake ni tani 1 hivi.
Roboti hii inaweza kufanya doria, kuchunguza, kusaidia mapambano, kufanya mawasiliano, na kusafirisha watu na vitu. Ina bunduki moja nyepesi yenye kipenyo cha milimita 7.62 na bunduki moja nzito yenye kipenyo cha milimita 12.7. Watafiti pia wanapanga kuweka mzinga mdogo kwenye roboti hii.
Askari wanaweza kuwasiliana na roboti hii kwa remote kwa umbali wa kilomita 3. Pia inaweza kuendeshwa kwa maneno au ishara ya mikono. Askari akitaka roboti hii kumsaidia, anatakiwa kupunga silaha yake kwa njia maalum, baadaye roboti inafyatulia risasi kitu au mtu aliyelengwa.
Mchana roboti hii inaweza kutambua shabaha iliyoko umbali wa kilomita 5 kutoka mahali ilipo kwa darubini, na usiku inaweza kutambua shabaha iliyoko kilomita 4 kwa kifaa cha kuonea usiku.
Roboti hii ina injini yenye nguvu kubwa, na inaweza kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 32 kwa saa. Inapofanya kazi ya usafirishaji, inaweza kubeba vitu vyenye uzito wa kilo 700.
Askari mmoja anaweza kuziongoza roboti 18 kufanya kazi kwa pamoja kwa remote moja tu.

Share:

Saturday, July 2, 2016

MWANAUME AZIRAI BAADA YA KUKUTANA NA MCHEPUKO WAKE FACEBOOK AMBAYE NI MWANAE

Kulitokea kizaazaa mapema wiki hii jijini Nairobi baada ya jamaa mmoja kujipata kwenye njia panda. Jamaa huyu amekuwa na mpenzi wa Facebook ambaye aliamua wakutane kwenye mojawalo ya  lodgings jijini.
Siku ya kukutana ilipofika, baba watoto akamhadaa mkewe kuwa ameenda biashara nje ya jiji na kuwa angerejea siku inayofuata. Asichojua mkewe ni kwamba, jamaa alikuwa anaenda kukutana na 'mpango wa kando'.

Nyumbani, jamaa ana watoto watatu,  akiwemo binti wa chuo kikuu. Binti huyu vile vioe akawadanganya wazazi wake kuwa alikuwa anaenda safari ya shule na hivyo apewe ruhusa. Kumbe lengo la binti huyu ni kukutana na 'mwanaume' wake wa Facebook.
Hapa, baba mtu hajajua kuwa huyu binti yake ndiye 'mpango wake wa kando'. Kisa na maana-WAMEKUWA WAKITUMIA PICHA BANDIA KWENYE FACEBOOK NA VILE VILE HAWAJAWAHI KUPIGIANA SIMU. WAO HUTUMIANA JUMBE TU KWENYE FACEBOOK.

Haya basi , mume akaaga familia yake, akiwemo msichana 'mpango wa kando' ambaye alitarajiwa kusafiri jioni 'safari ya shule'.
Baada ya kufika kwenye lodging, baba mtu akamtumia mrembo ambaye kwenye 'picha' za Facebook, alikuwa ameumbwa akaumbika. Si kiuno, si makalio, si sura, si ngozi laini, si macho ya gololi, nakadhalika, ujumbe wa kumwelekeza kwenye chumba cha kulala.

Baba mtu akaitisha chakula ndani ya chumba huku akisubiri windo lake. Mzee wa wenyewe akaoga, kuhakikisha kuwa hanuki jasho. Akajipuliza manukato... Yote kwa matayarisho ya kumpokea 'mgeni'. Mzee alikuwa amemtumia ujumbe mrembo na kumwelekeza kulikokuwa chumba. Baada ya saa kadhaa za kusubiri kwa hamu na hamumu, mtoto wa wenyewe akawasili. Akaelekea moja kwa moja hadi kwenye chumba alichokuwa ameelekezwa na 'mchumba' wake.

Msichana akabisha mlango wa chumba. Baba mtu akajinyoosha, tayari kumlaki mgeni. Alipofungua mlango, amini usiamini alizirai. Mwanamke aliyekuwa akimtarajia ni binti yake. Aibu gani hii!!! #MapenziYaFacebook

Share:

Thursday, June 30, 2016

JPM ATENGUA UTEUZI WA MA-DC WATATU WAKATI WA KUAPISHWA


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya watatu huku mmoja akiwa amebakiza muda mfupi kabla ya kula kiapo cha uadilifu, Ikulu, Dar es Salaam.Imegundulika kuwa wawili waliteuliwa kimakosa na mmoja tayari ana wadhifa mwingine wa ubunge.Akitoa ufafanuzi juu ya hatua hiyo Ikulu Dar es Salaam jana, wakati wa kuapisha wakuu wa mikoa wapya watatu na shughuli ya kula kiapo cha uadilifu kwa ma-DC wapya 139, Dk Magufuli alisema alitengua uteuzi wa Fikiri Avias Said kwa kuwa jina lake lilikosewa.Alisema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi mkoani Singida ni Miraji Mtaturu. Mtaturu alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza.
Aidha, Dk Magufuli alisema ametengua uteuzi wa Fatma Toufiq kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa kuwa tayari mteule huyo ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Badala yake, nafasi hiyo imezibwa na Agnes Hokororo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho tawala. Katika Serikali ya Awamu ya Nne, Toufiq alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.“Nilishasema katika utawala wangu, kila kazi itakuwa na mtu mmoja ili kuwe na ufanisi katika utendaji. Mtu mmoja, kazi moja,” alisisitiza Rais Magufuli akifafanua kuhusu Fatma Toufiq.

Share:

KUTANA NA TEKNOLOJIA YA KUCHAJI SIMU 8 BILA WAYA


Teknolojia ya kuchaji bila waya bado haitumiki sana, kwa sababu kuchaji kwa njia hii kunahitaji muda, tena vyombo vichache tu vya elektroniki vinatumia teknolojia hii. Hivi karibuni kampuni moja imetangaza chombo kipya cha kuchaji bila waya kiitwacho "Fli Charge". Kinaweza kuchaji simu yako kwa kasi na ufanisi mkubwa, hata huna haja ya kuweka simu yako kwenye ubao wa kuchaji. Kampuni hiyo pia imetengeneza plagi maalum kwa microUSB na kwa simu za IPhone, hivyo simu za kawaida aina ya smartphone pia zinaweza kuchajiwa na chombo hiki kwa kuunganishwa na plagi hizi, Chombo hiki kinatoa Watt 40 za umeme, kinaweza kuchaji simu 8 kwa wakati mmoja. Hii ni habari nzuri kwa watu wenye simu nyingi. Lakini ukichaji simu nyingi zaidi kwa wakati mmoja, ufanisi wake unapungua. Hivi sasa kampuni yake inakusanya uwekezaji kwenye tovuti ya Indiegogo, inapanga kukusanya dola za kimarekani laki moja ili kuzalisha chombo hiki. Lengo hili likitimizwa, chombo hiki kinatazamiwa kuanza kuuzwa mwezi Oktoba mwaka huu. CRI Kiswahili's photo.
Share:

Wednesday, June 29, 2016

MAHAKAMA YATENGUA UBUNGE WA MBUNGE WA CHADEMA



Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua ushindi wa Mbunge wa Longido (Chadema), Onesmo Ole Nangole baada ya kujiridhisha kuwa mazingira katika chumba cha majumuisho ya kura hayakuwa rafiki kuakisi matakwa ya wapiga kura.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Sivangilwa Mwangesi amesema amefikia uamuzi huo na kumtaka mlalamikiwa kulipa gharama za kesi hiyo licha ya kutupa ushahidi wa mashahidi wa mlalamikaji 15 na kukubali wa wanne.
Amesema pia kuwa hata kura zenye makosa hazikufikia alizopata mshindi.
Baada ya hukumu hiyo, Ole Nangole amesema alishinda kwa halali na anakusudia kukata rufaa huku mshindi wa kesi hiyo, Steven Kiruswa akisema mahakama imetenda haki.


Share:

TANAPA SASA YAIKUMBUKA KIGOMA




 Mahale

Kigoma. Baada ya kuteseka muda mrefu, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) inatarajia kuanza ujenzi wa madaraja manne yakatayounganisha barabara kuu ya Mahale hadi mji wa Kigoma.
Hivi sasa watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mahale wanalazimika kusafiri kwa siku mbili majini kutoka Kigoma Mjini, huku wananchi wakitumia muda huohuo kutoka Mahale hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Uvinza yaliyopo mjini Kigoma.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi wa maeneo hayo hawawezi kwenda mjini na wakiamua kwenda inawalazimu kupanda boti Ziwa Tanganyika na kusafiri kwa siku hizo kutokana na ukosefu wa barabara, suala linalosababisha wakose fursa nyingi za uchumi.
Madaraja hayo yanajengwa kwenye kipande cha barabara chenye urefu wa kilomita 38 katika kata za Buhingu, Kalyia na Igalula wilayani Uvinza kwa gharama ya Sh1.84 bilioni.

Share:

TANZANIA NA COMORO ZAAHIDIANA USHIRIKIANO SEKTA MBALIMBALI

Times Fm TZ's photo.

Rais Azali Assoumani wa Comoro amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na biashara.Alitoa kauli hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Umrah.Amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za kijamii na kusisitiza serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Comoro.
Akitoa ujumbe wa Rais Magufuli kwa Rais Assoumani, Makamu wa Rais Samia amemhakikishia rais huyo wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais Assoumani kheri katika safari yake ya Makka kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Share:

DARAJA REFU NA LA KALE ZAIDI DUNIANI HILI HAPA


Daraja la Anping mjini Jinjiang ambalo pia linaitwa ‘Wuliqiao’ lina urefu wa maili 5 za kichina, lina sifa ya kuwa daraja lenye umbali mrefu zaidi duniani. Ujenzi wake ulianza mwaka 1138 AD, na ulichukua miaka 14 kukamilika. Daraja hili sio tu ni refu zaidi duniani kutoka zamam za Kati, bali pia ni daraja la kale zaidi lililojengwa kwa mawe ambalo bado linatumika nchini China. Ujenzi wa daraja hili ulifanya bandari ya Anhai Nangang kuwa moja ya bandari kuu mjini Quanzhou, pia ni alama ya wazi ya biashara ya nje ya Jinjiang kupitia Njia ya Hariri ya Baharini.




Share:

RIPOTI YA LUGUMI KUWASILISHWA BUNGENI MKUTANO UJAO WA BUNGE



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu

Dodoma. Ripoti ya sakata la mkataba wa Kampuni ya Lugumi Enteprises na Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa mkutano ujao.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.
Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.

Share:

LISSU APUNGUZIWA MASHTAKA MAWILI




Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amefutiwa mashtaka mawili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria.
Lissu alipandishwa jana na kusomewa mashtaka ya uchochezi, huku akiunganishwa na wenzake watatu.
Mashtaka yaliyofutwa ni la kwanza na la tatu, kwa kile kilichodaiwa kuwa yalipaswa kuambatana na hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za upande wa mashtaka na utetezi.

Share:

WANUFAIKA WA ESCROW HAWAKO SALAMA-MLOWOLA




Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema watu waliopokea mgawo wa fedha zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, hawako salama kwani anaendelea kuchunguza nyaraka.
Amesema uchunguzi wa sakata hilo la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo unahitaji umakini mkubwa, ukikamilika wote watakaobainika watachukuliwa hatua.
Mawaziri wawili (Profesa Sospeter Muhongo na Profesa Anna Tibaijuka), waliwajibika kutokana na sakata hilo, viongozi wa kamati za Bunge (Andrew Chenge, William Ngeleja na Victor Mwambalaswa) kuvuliwa madaraka, wanasiasa kufikishwa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na watumishi wengine kufikishwa mahakamani.
Chenge na Profesa Tibaijuka waliwajibishwa kutokana na kuonekana wameingiziwa Sh1.6 bilioni kila mmoja kwenye akaunti zao, Ngeleja (Sh40.4 milioni), wakati Mwambalaswa aliwajibika kutokana na mgongano wa kimaslahi.

Share:

MAKONDA AVUTANA NA HALMASHAURI KUHUSU KAMPUNI ZA UJENZI



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Dar es Salaam. Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizuia Kampuni ya Ujenzi ya Delmont kupewa zabuni upya jijini hapa hadi atakapojiridhisha, Kamati ya Fedha ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, imeiruhusu kumalizia kazi iliyoianza.
Juni 24, Makonda alisitisha utoaji upya wa zabuni kwa kampuni nne za makandarasi ikiwamo ya Delmont, kwa kile alichodai zina uwezo mdogo wa ujenzi.
Kamati hiyo ikiongozwa na Meya wa manispaa hiyo, Boniface Jacob ilitoa uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kukagua barabara ya Mabatini hadi Kijitonyama inayodaiwa kujengwa chini ya kiwango na kampuni hiyo.
Mhandisi wa Delmont, Salutari Mushi alisisitiza kuwa hawana makosa na wanafanya kile walichoelekezwa na wahandisi kupitia mwongozo na michoro ya usanifu.
Share:

DRONE YA MAREKANI YAANGUKIA MIKONONI MWA AL-SHBAAB



Ndege moja isiokuwa na rubani inayodaiwa kumilikiwa na Marekani imeanguka kusini mwa Somalia kulingana na chombo cha habari cha Shabelle. Chombo hicho kinasema kuwa ndege hiyo yenye kamera za kuchunguza ilianguka siku ya Jumanne katika eneo la Baladul-Amin eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa al-Shabab katika jimbo la Shabelle. Ripoti zinasema kuwa wapiganaji wa al-Shabab walielekea pale ndege hiyo ilipoanguka na kuchukua mabaki yake.
Share:

SMARTPHONE YA BEI RAHISI DUNIANI YAZINDULIWA INDIA

Kupata simu ya bei rahisi zaidi duniani aina ya smartphone sio rahisi.
Freedm 251 ni simu ya Android iliotengazwa na kampuni ya Ringing Bells kutoka India na inagharimu Rupee 251 sawa na pauni 2.77.
Unapoibeba kwenye mkono utahisi umebeba simu ya kampuni ya Apple aina ya iPhone 5.
Na kulingana na bei yake ina programu za kuvutia.
  • Kamera ya mbele na nyuma.
  • Ina upana wa nchi nne.Ina programu ya Quad-core inayotoa nguvu ya operesheni ya simu hiyo lakini haitumii betri yake mara nyengine.
Kuna aina mbili moja ya simu hizo nyeusi na moja nyeupe.Unapoitumia inafanya kazi kama smartphone ya kawaida.
Hatahivyo ni vigumu kuipima uwezo wake kwa kuwa ina programu chache ambazo hufanya kazi za kawaiada.
Share:

UKAWA WATISHIA KUMPELEKA JPM ICC




Wabunge wa Ukawa

Dodoma. Wabunge wa Ukawa wamemtaka Rais John Magufuli kutoa tamko juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar na kwamba, wana mpango wa kumpeleka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakidai yanayotokea visiwani humo yana baraka zake.
Katika mkutano wao na wanahabari jana, wabunge hao wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwenda Zanzibar kujionea hali halisi badala ya kupata taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.
Hata hivyo, CCM imesema inalaani tamko hilo na kuwa kama Ukawa wanaona kuna masuala yanayohitaji kurekebishwa na kuhitaji hatua za haraka za Serikali watumie vyombo vinavyotambulika kisheria kama Bunge badala ya kuishia kulalamika “vichochoroni”.
Akitoa tamko la wabunge hao jana, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alieleza kuwa hali ya kiusalama inazidi kuwa mbaya Pemba na Unguja baada ya uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kutokana na baadhi ya wananchi kupigwa na vikosi alivyodai ni vya usalama.

Share:

Tuesday, June 28, 2016

AFUNGWA JELA KWA UDANGANYIFU WA MTIHANI


Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.
Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.
Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.
Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.
Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.
Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto.
Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.
Share:

KITWANGA HADHARANI BAADA YA KIMYA KIREFU


Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba

Dar es Salaam. Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ameibuka na kukabidhi ofisi na akatoa ratiba ya shughuli zake katika Jimbo lake la Misungwi ikiwamo ibada ya shukrani.
Kitwanga, ambaye uwaziri wake ulitenguliwa Mei 20 na Rais John Magufuli, baada ya kuingia na kujibu swali bungeni akiwa amelewa, alikabidhi ofisi jana kwa Mwigulu Nchemba ambaye amechukua nafasi yake.
Baada ya kutenguliwa uteuzi wake, hakuwahi kuonekana hadharani kwa maelezo kuwa alikuwa amekwenda Israel kwa ajili ya shughuli zake.

Share:

RASILIMALI NYINGINE YAGUNDULIKA TANZANIA

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Share:

WAFAHAMU WAPINZANI WA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO

Yanga imeingia kambia nchini Uturuki kwa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo za makundi
Zimebaki siku chache kabla ya mabingwa wa Tanzania bara Yanga kutupa karata ya kwanza kwenye kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, Yanga imeingia kambia nchini Uturuki kwa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo za makundi, na tayari benchi la ufundi limeanza boresha timu kwa kuongeza wachezaji kama Kessy, Vicent Adrew, Juma Mahadhi na Ben Kakolanya
Goal inakuchambulia wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya makundi shirikisho Afrika
Tp Mazembe
Timu kutoka Congo imeanzishwa mwaka 1939, ni mabingwa mara tano wa klabu bingwa Afrika , timu inayo milikiwa na tajiri wa madini nchini Congo Moise Katumbi Tp Mazembe  wanatumia uwanja wao wa Stade duTp Mazembe unachukua watazamaji 18500, vijana wa kocha Hubert Velud wanaongoza ligi kuu nchini mwao baada ya michezo 9 wamejikusanyia pointi 23 tatu zaidi ya timu inayowafuatia. Wamekusanya wachezaji wazoefu kwenye michuano hii kama Kidiaba, Singuluma na Kasusula. Mtu ambaye ni tegemezi kwenye timu hii Adama Traore raia wa Mali na Roger Assale raia wa Ivory Coast.
Mo Bejaia
Timu kutoka Algeria imeanzishwa mnamo mwaka 1954, si timu maarufu Afrika na hata nchini mwao hawana historia kubwa zaidi ya kuchukua ubingwa wa Fa 2015 wanatumia uwanja wa Stade I’unite Maghrebine uliopo mji wa Bejaia unachukua watazamaji 19000 tu, wako nafasi ya sita kwenye ligi yao baada ya michezo 30 wamejikusanyia alama 44. Wachezaji wao hatari ni Mouhamed Ndoye raia wa Senegal anayecheza kiungo cha kushambulia na Zahir Zerdab.
Medeama Sc
Kwenye kundi hili hii ndiyo timu changa kuliko zote imeanzishwa mwaka 2002 nchini Ghana katika mji wa Tarkwa, uwanja wao wa nyumbani wa Tarkwa T & A Park unachukua watazamaji 5000 na ni timu pekee inayonolewa na mzawa katika kundi hili Bw. Prince Owusu raia wa Ghana, wanashika nafasi ya tano kwenye timu 16 ligi kuu ya Ghana baada ya kujikusanyia alama 26 kwenye michezo 15 pointi mbili zaidi na anaeongoza ligi nchini mwao. Si timu kubwa kwenye ukanda huu wa Afrika na haina historia yeyote kwenye michuano hii, kikubwa wanacho jivunia ni ubingwa wa Super Cup walio upata mwanzoni wa mwaka huu. Mtu ambaye ambaye yupo nyuma ya mafanikia yao ni kiungo Kwesi Donsu na mshambuliaji mdogo Bismack Oppong.

Share:

WIMBI LA WACHEZAJI KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA LAZIDI KUIANDAMA ARGENTINA


Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina, baada ya kushindwa kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chile, wachezaji wa Argentina mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakitangaza kustaafu kuichezea timu yao ya taifa.
Mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo alikuwa Leo Messi ambaye alitangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya Chile kumalizika.
Muda mfupi baadae mshambuliaji wa klabu ya ya Manchester City, Sergio Aguero na mlinzi wa kati wa FC Barcelona Javier Mascherano nao pia walitanga kuachana na soka la kimataifa.
Kama vile haitoshi, ripoti kutoka Amerika ya Kusini zinadai kuwa, Angel Di Maria, Ezequiel Lavezzi, Gonzalo Higuain na Lucas Biglia nao pia wameamua kutundika daruga kuitumikia Argentina.
Laikini kocha wa timu hiyo Tata Martino hajachukua uamuazi wa kuikacha timu hiyo.

Share:

Monday, June 27, 2016

MWIJAGE KUIFUFUA GENERAL TYRE

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage haishiwi mbwembwe sasa amekuja na mpango wa kufufua kiwanda cha kutengeneza matairi ya magari cha General Tyre, kwa kununua mashine mpya za kisasa.
Hivi karibuni, Mwijage alitangaza kuwa baada ya miaka mitano mtu atakayevaa nguo kutoka nje azomewe mitaani, kwani viwanda vya ndani vitakuwa vimeanza uzalishaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mwijage alisema wataalamu wametumwa nje ya nchi kufanya utafiti wa mashine mpya za kutengeneza matairi.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliitaka Serikali kuharakisha kukifufua kiwanda hicho, kwani kina uwezo wa kutoa ajira nyingi kwa vijana.

Share:

MESSI ASTAAFU KWA UCHUNGU CHILE KUCHUKUA UBINGWA

Chile mabingwa Copa America
Fainali ya tano kwa Argentina na Lionel Messi bila taji! Kwa mara nyingine dhidi ya Chile Argentina wameshindwa kuonyesha umahiri wao katika upigaji penalti.

Katika mechi iliyokuwa imetawaliwa na faulo nyingi kipindi cha kwanza, ikiwa ni pamoja na kadi nyekundu kwa wachezaji wawili, kila timu ikipata moja, mechi ilienda hadi dakika za nyongeza baaa ya dakika tisini kuisha bila goli baina ya pande zote, hatimaye mikwaju ya penalti. Ni Francisco Silva aliyepiga penalti ya ushindi na kuipatia Chile ubingwa Copa America.
Faustino Marcos Alberto Rojo alipata kadi nyekundu dakika ya 43 baada ya Marcelo Alfonso Díaz Rojas kuoneshwa kadi ya pili ya njano.
Hata hivyo, Silva asingeweza kuipatia ubingwa timu yake kama si Claudio Bravo aliyeonyesha umahiri wake kwa kuokoa penalti moja pia Messi akikosa.
Bravo aliokoa tena mpira wa adhabu uliopigwa dakika ya 10 katika muda wa nyongeza kutoka umbali wa yadi 35. Shuti la Messi liliingia ndani ya boksi kidogo mpira uzame wavuni karibu na kugonga besela. Bravo aliugusa na kuutoa nje. Jambo la kushangaza kwa umahiri wake!
Kisha, baada ya muda wa ziada, Argentina walikuwa na nafasi kubwa zaidi kwani Chile walikosa penalti ya kwanza. Hiyo ilimwacha Messi na fursa ya kumshangaza Bravo na kuiweka timu yake mbele lakini ikawa kinyume. Alikosa!
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukosa tuta katika mikwaju ya penalti.
Fainali ya tano kwa Messi bila kombe, hali kadhalika maumivu na majuto makubwa kwa Javier Mascherano na Sergio Aguero. Hawana bahati!
Share:

PROFESA WA UDSM NA BOSI WA SUMATRA AJIUA KWA RISASI



Profesa Mkilaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idd Mkilaha, inadaiwa amefariki dunia jioni hii nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam baada ya kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, amekufa kwa kujipiga risasi, lakini tunachunguza kubaini kama ilikuwa ni bahati mbaya au alidhamiria kufanya hivyo,” amesema Sirro.
Hata hivyo, amesema taarifa zaidi atazitoa kesho.
Profesa Mkilaha alikuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Share:

Sunday, June 26, 2016

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAPYA HAWA HAPA

TAARIFA: RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA WILAYA 139 NA KUFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA WATATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.

Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.

Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)

ARUSHA

Arusha –           Mrisho Mashaka Gambo
Arumeru –           Alexander Pastory Mnyeti
Ngorongoro –           Rashid Mfaume Taka
Longido –           Daniel Geofrey Chongolo
Monduli –           Idd Hassan Kimanta
Karatu –           Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM

Kinondoni –           Ally Hapi
Ilala –           Sophia Mjema
Temeke –           Felix Jackson Lyaviva
Kigamboni –           Hashim Shaibu Mgandilwa
Ubungo –           Hamphrey Polepole
DODOMA

Chamwino –           Vumilia Justine Nyamoga
Dodoma –           Christina Solomon Mndeme
Chemba –           Simon Ezekiel Odunga
Kondoa –           Sezeria Veneranda Makutta
Bahi –           Elizabeth Simon
Mpwapwa –           Jabir Mussa Shekimweli
Kongwa –           John Ernest Palingo
GEITA

Bukombe –           Josephat Maganga
Mbogwe –           Matha John Mkupasi
Nyang’wale –           Hamim Buzohera Gwiyama
Geita –           Herman C. Kipufi
Chato –           Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA

Mufindi –        Jamhuri David William
Kilolo –           Asia Juma Abdallah
Iringa –           Richard Kasesela
KAGERA

Biharamulo –           Saada Abraham Mallunde
Karagwe –           Geofrey Muheluka Ayoub
Muleba –           Richard Henry Ruyango
Kyerwa –           Shaban Ilangu Lissu
Bukoba –           Deodatus Lucas Kinawilo
Ngara –           Col. Michael M. Mtenjele
Missenyi –           Col Denis F. Mwila
KATAVI

Mlele –           Rachiel Stephano Kasanda
Mpanda –           Lilian Charles Matinga
Tanganyika –           Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA

Kigoma –           Samsoni Renard Anga
Kasulu             –           Martin Elia Mkisi
Kakonko –           Hosea Malonda Ndagala
Uvinza             –           Mwanamvua Hoza Mlindoko
Buhigwe –           Elisha Marco Gagisti
Kibondo –           Luis Peter Bura
KILIMANJARO

Siha –           Onesmo Buswelu
Moshi –        Kippi Warioba
Mwanga –     Aaron Yeseya Mmbago
Rombo –       Fatma Hassan Toufiq
Hai –           Gelasius Byakanwa
Same –        Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI

Nachingwea –           Rukia Akhibu Muwango
Ruangwa –           Joseph Joseph Mkirikiti
Liwale –           Sarah Vicent Chiwamba
Lindi –           Shaibu Issa Ndemanga
Kilwa –           Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA

Babati –           Raymond H. Mushi
Mbulu –           Chelestion Simba M. Mofungu
Hanang’ –           Sara Msafiri Ally
Kiteto –           Tumaini Benson Magessa
Simanjiro –           Zephania Adriano Chaula
MARA

Rorya –           Simon K. Chacha
Serengeti –           Emile Yotham Ntakamulenga
Bunda –           Lydia Simeon Bupilipili
Butiama –           Anarose Nyamubi
Tarime –           Glodious Benard Luoga
Musoma –           Vicent Anney Naano
MBEYA

Chunya –           Rehema Manase Madusa
Kyela –           Claudia Undalusyege Kitta
Mbeya –           William Ntinika Paul
Rungwe –           Chalya Julius Nyangidu
Mbarali –           Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO

Gairo –           Siriel Shaid Mchembe
Kilombero –           James Mugendi Ihunyo
Mvomero –           Mohamed Mussa Utali
Morogoro –           Regina Reginald Chonjo
Ulanga             –           Kassema Jacob Joseph
Kilosa –           Adam Idd Mgoyi
Malinyi –           Majula Mateko Kasika
MTWARA

Newala –           Aziza Ally Mangosongo
Nanyumbu –           Joakim Wangabo
Mtwara –           Khatibu Malimi Kazungu
Masasi –           Seleman Mzee Seleman
Tandahimba –           Sebastian M. Walyuba
MWANZA

Ilemela –           Leonald Moses Massale
Kwimba –           Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
Sengerema –           Emmanuel Enock Kipole
Nyamagana –           Mary Tesha Onesmo
Magu –           Hadija Rashid Nyembo
Ukerewe –           Estomihn Fransis Chang’ah
Misungwi –           Juma Sweda
NJOMBE

Njombe –           Ruth Blasio Msafiri
Ludewa             –           Andrea Axwesso Tsere
Wanging’ombe –           Ally Mohamed Kassige
Makete             –           Veronica Kessy
PWANI

Bagamoyo –           Alhaji Majid Hemed Mwanga
Mkuranga –           Filberto H. Sanga
Rufiji –           Juma Abdallah Njwayo
Mafia –           Shaibu Ahamed Nunduma
Kibaha –           Asumpter Nsunju Mshama
Kisarawe –           Happyness Seneda William
Kibiti –           Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA

Sumbawanga –           Khalfan Boniface Haule
Nkasi –           Said Mohamed Mtanda
Kalambo –           Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA

Namtumbo –           Luckness Adrian Amlima
Mbinga –           Cosmas Nyano Nshenye
Nyasa –           Isabera Octava Chilumba
Tunduru –           Juma Homela
Songea –           Polet Kamando Mgema
SHINYANGA

Kishapu –           Nyambonga Daudi Taraba
Kahama –           Fadhili Nkulu
Shinyanga –           Josephine Rabby Matiro
SIMIYU

Busega –           Tano Seif Mwera
Maswa –           Sefu Abdallah Shekalaghe
Bariadi –           Festo Sheimu Kiswaga
Meatu –           Joseph Elieza Chilongani
Itilima –           Benson Salehe Kilangi
SINGIDA

Mkalama –           Jackson Jonas Masako
Manyoni –           Mwembe Idephonce Geofrey
Singida –           Elias Choro John Tarimo
Ikungi –           Fikiri Avias Said
Iramba –           Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE

Songwe –           Samwel Jeremiah
Ileje –           Joseph Modest Mkude
Mbozi –           Ally Masoud Maswanya
Momba –           Juma Said Irando
TABORA

Nzega –           Geofrey William Ngudula
Kaliua –           Busalama Abel Yeji
Igunga –           Mwaipopo John Gabriel
Sikonge –           Peres Boniphace Magiri
Tabora –           Queen Mwashinga Mlozi
Urambo –           Angelina John Kwingwa
Uyui –           Gabriel Simon Mnyele
TANGA

Tanga –           Thobias Mwilapwa
Muheza –           Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
Mkinga –           Yona Lucas Maki
Pangani –           Zainab Abdallah Issa
Handeni –           Godwin Crydon Gondwe
Korogwe –           Robert Gabriel
Kilindi –           Sauda Salum Mtondoo
Lushoto –           Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

Share:

ONE-THIRD OF DEVELOPING WORLD HOSPITALS LACK RUNNING WATER


More than one-third of hospitals in the developing world lack running water, a deficiency that can lead to unsanitary conditions for patients in general and dangerous conditions for those who need surgery, says a study covering 430 hospitals in 19 countries.

“Running water is something we so take for granted and it doesn’t exist in a third of hospitals in these countries,” said one of the lead researchers Adam Kushner, Adjunct Professor at Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health in Baltimore, Maryland, US.

“Instead of water just being there, some hospitals truck in water or collect it in rain barrels, with no guarantee of its cleanliness. Without clean water, there is no way to clean surgeons’ hands or instruments, wash gowns and sheets or clean wounds to prevent or reduce infections,” Kushner said.

For their study, the researchers analysed published research related to surgical capacity in low- and middle-income countries.

They identified 19 surgical capacity studies undertaken between 2009 and 2015 that included information on water availability covering 430 hospitals in 19 nations.

The researchers found that 34 per cent of the hospitals — 147 of the 430 — lacked continuous running water.

These ranged from less than 20 per cent with running water in Liberia to more than 90 per cent in Bangladesh and Ghana.

The findings were published online in the Journal of Surgical Research.

Many people in the world — an estimated 700 million — live without access to water; half of those without water live in sub-Saharan Africa.

Lack of access to water and sanitation has a significant negative impact on health care provision, including surgical care, the researchers noted.
Share:

Saturday, June 25, 2016

MWIZI SUGU WA MAJENEZA KENYA ANENA KUTOKA GEREZANI

CRI Kiswahili's photo.












Aliyekuwa jambazi sugu na mwizi wa majeneza jijini Nairobi John Kibera ameshindwa kuhudhuria mazishi ya mtu yoyote .
Licha ya kutumikia kifungo chake baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kufukua na kuiba majeneza kabla ya kuyaauza,Kibera amesema sasa hata familia yake inaogopa kumuona kwenye mazishi.
John amesema kwa sasa yeye ameokoka na hafanyi tena uhalifu huo .

Amepeana kwa mayatima nyumba ya shilingi milioni 7 aliyonunua kwa pesa za kuuza majeneza .
Zama zake alikuwa mmoja kati ya majambazi sugu waliosakwa na polisi kote nchini.
Share: