Sadiq Khan Mwingereza mwenye asili ya Pakistan ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo na wapinzani zaidi ya wawili, amefanikiwa kushinda umeya kwa asilimia 56.8 akifuatiwa kwa karibu na mshindani wake mkuu Tory Zac Goldsmith ambaye amefanikiwa kupata asilimia 43.2.
Bwana Khan ni mwana wa dereva wa zamani wa bas jijini London aliyezaliwa Pakistan
Sadiq Khan mwenye umri wa miaka 45 anakuwa Meya wa kwanza Mwislamu kuiongoza London katika historia ya mji huo. Mwanasiasa huyo wa chama cha Lebour ni watetezi wa fijkra ya kujitoa Uigereza katika Umoja wa Ulaya.
Kwa matokeo hayo Sadiq Khan atachukua kiti cha Umeya wa London akimrithi Boris Johnson Meya mwenye makelele mengi ambaye analazimika kukiachia kiti hicho baada ya kukikalia kwa miaka minane.
Wasimamizi wa kampeni ya mpinzani wake katika uchaguzi huo Zac Goldsmith, ambaye ni tajiri mkubwa walishutumiwa kwa kudai kuwa Bwana Khan ana uhusiano na Waislamu wenye itikadi kali.
Bwana Khan alisema kuwa wakaazi wa London wamepiga kura ya umoja na kuponza mgawanyiko.
Ushindi huo ni wa kumtia moyo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn.
Chama chake kilipata ushindi dhaifu katika maeneo mengine ya nchi katika uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment