Search This Blog

Wednesday, May 4, 2016

ZIMBABWE YAAMUA KUWAUZA WANYAMAPORI, SABABU KUU YATAJWA


Mamlaka ya Uendeshaji Mbuga za Wanyama na Wanyama Pori imewatangazia wananchi kuwa wale wote wenye uwezo wa kununua na kuwashughulikia wanyama pori pamoja na kuwa na ardhi ya kutosha ya kuwaweka wanyama hao wawasiliane na mamlaka hiyo kwa ajili ya kujisajili.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu wanyama wanaouzwa au bei zao, lakini mbuga 10 za taifa za wanyama za nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ni maarufu kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, simba, vifaru, chui na nyati.
Ukame uliolikumba eneo la kusini mwa Afrika umewafanya raia zaidi ya milioni nne wa Zimbawe wahitajie msaada wa chakula pamoja na kuathiri mazao yao wanayohitajia kwa chakula na uuzaji nje ya nchi kwa ajili ya kipato, kuanzia mahindi hadi tumbaku.
Imeelezwa kuwa uuzaji wanyama pori utasaidia baadhi ya wanyama hao kupata makazi mapya pamoja na kupunguza makali ya uhaba wa fedha unaozikabili mbuga za taifa za wanyama ambazo zinasema zinapokea fungu dogo la fedha kutoka serikalini.
Msemaji wa mamlaka ya mbuga za wanyama Caroline Washaya-Moyo hajaeleza kama wanyama hao wanaweza pia kuuzwa nje ya nchi ikikumbukwa kuwa makundi yanayotetea wanyama pori yalitoa malalamiko makali mwaka jana wakati Zimbabwe iliposafirisha tembo 60 nje ya nchi, nusu yao wakipelekwa nchini China ambako inasemekana wana bei ya juu kutokana na matumizi ya pembe zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment