Wanachama wa chama cha Republicans nchini Marekani wametofautiana kuhusu kumuunga mkono mgombea wa urais wa chama hicho Donald Trump baada ya mfanyibiashara huyo kushinda uteuzi wa chama hicho.
Baadhi ya wanachama hao wameandika katika mitandao ya kijamii kuhusu kujiondoa kwao katika chama hicho kupitia kuchoma vibali vyao vya kupiga kura.
Hatahivyo wengine wameanza kumuunga mkono mgombea huyo wakisema kuwa bw Trump anapendwa sana kushinda Hillary Clinton ambaye anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa chama cha Demokrat.
Bwana Trump hana umaarufu mongoni mwa wapiga kura wengi nchini Marekani.
''Iwapo tutamteua Trump,tutaharibikiwa na itakuwa kupenda kwetu'',Seneta wa jimbo la Carolina Lindsay Grahama alisema siku ya Jumanne baada ya Seneta wa Texas Ted Cruz kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho na hivyobasi kumpatia bw Trump fursa.
Wengine kama vile aliyekuwa gavana wa jimbo la Louisiana Bobby Jindal ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bw Trump katika siku za nyuma amesema kuwa atamuunga mkono katika uchaguzi ujao.
0 comments:
Post a Comment