Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited, inakanusha taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari siku ya jana na leo kwa baadhi ya Magazeti kuwa imeficha sukari ambayo inatakiwa kwa matumizi ya kawaida majumbani.
Utoaji taarifa wa aina hii ambao haukuzingatia ukweliunachochea hasira za wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kupungua kwa sukari ya majumbani katika soko la hapa nchini.
Mohamed Enterprises pamoja na kuwa kampuni ya biashara kimataifa ikiuza bidhaa za kilimo na kununua, pia inajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa ambazo zinahitaji sukari ya kiwandani.
Bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji baridi. Ndio kusema katika muda wowote ule tunahitaji kuwa na akiba ya kutosha ya sukari hiyo kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Ifahamike Tunapoagiza sukari ama kwa mahitaji ya viwanda vyetu kampuni ya Mohamed Enterprises hufuata taratibu zote za Nchi.
Aidha sukari tani 2,990 zilizokutwa Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam, si mali ya MeTL bali ni mali ya kampuni ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji. Sisi tunachoelewa ni kwamba mzigo ulikuwa njiani kuelekea Uganda, lakini kutokana na uhaba wa sukari hapa nchini, Serikali iliruhusu mzigo huo kubaki nchini na ili kuingiza sokoni mara moja kati ya Mei 12 na Mei 13
“Tulifuata taratibu zote ikiwemo Mamlaka husika za Nchi Bodi ya Sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
Kwa mantiki hiyo, si sahihi kusema sukari tunayoiagiza nchini ni ya kiwango duni wakati hukaguliwa na mamlaka zote husika za kiserikali ikiwemo TFDA na TBS. Pia kauli kuhusu sukari kuagizwa toka Brazil na kufanyiwa ‘repackaging; Nchini Dubai suala hilo ni jambi la kawaida
“Kampuni yetu huagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa sukari wa Dubai kutokana na lojistiki zinavyoruhusu.
Kuagiza sukari kutoka Brazil na kuisafirisha hadi Tanzania ni siku 50 hadi 60 kwa njia ya meli, lakini kutoka Dubai ni siku 7 tu, kwa mtu anayefanya biashara lazima ataagiza sukari kutoka Dubai, kuna maslahi zaidi katika hesabu za kibiashara.
Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi si wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai.
Ofisi zetu zipo Dar Es Salaam Tanzania, na uongozi upo wazi, laiti kama tungelitafutwa na kuulizwa tungeliweza kutoa maelezo yaliyojitosheleza, kuepusha mikanganyiko na kuweka habari katika mizania inayostahili.
Tunazo nyaraka zote zinazothibitisha uhalali wake ikiwemo TRA, TFDA na Bodi ya Sukari, hivyo hakukuwa na haja kufichwa sukari hiyo kwa sababu zozote zile.
Pia, ieleweke tatizo hilo la sukari ilishaagizwa ya kutosha na itafurika nchi nzima ndani ya wiki mbili zijazo, hivyo Watanzania hawapaswi kuwa na hofu hiyo ya uhaba wa sukari.
0 comments:
Post a Comment