Search This Blog

Monday, April 25, 2016

JUHWATA YAWAONYA WANAOSUSIA VIKAO BUNGENI


Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Katibu wa JUHWATA bwana Mtela Mwampamba amesema kimsingi serikali ya awamu ya tano imekuwa na ari ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu pamoja na kiu ya kutatua kero za wananchi kwa kubana matumizi, hivyo wabunge kupinga na kuhujumu waziwazi jitihada hizo kwa maslahi yao binafsi ni masikitiko makubwa kwa jukwaa hilo.
Aidha, Mtela Mwampamba amesema kususia uamuzi wa Rais kuelekeza fedha zilizotakiwa kutumiwa na wabunge kukagua majengo ya balozi za Tanzania nje ya nchi na kuzielekeza katika ununuzi wa madawati 600 kwa kila jimbo pamoja na maamuzi mengine, Rais anaruhusiwa kikatiba ndani ya miezi kadhaa baada ya kuchaguliwa kuweza kubadili matumizi ya fedha.
JUHWATA imewataka wabunge kuelekeza dhamira zao katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano na mijadala isiyo na tija, kejeli na mipasho na kutekeleza ahadi zao kwa wananchi na kutoa ushirikiano kwa Rais katika juhudi za kuleta maendeleo kwa taifa.
Kuhusiana na suala la kurusha majadiliano ya bunge moja kwa moja (Live), JUHWATA imesema zama zimebadilika na kuwa kinachoendelea sio kunyima uhuru wa habari na kushauri serikali kuacha kurusha matangazo ya moja kwa moja hata katika shuguli zake za ufunguzi wa miradi au kukamilika kwa miradi kama ilivyofanya katika uzinduzi wa daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge)
Share:

0 comments:

Post a Comment