Search This Blog

Thursday, April 28, 2016

MAGUFULI AMEKAMILISHA KUUNDA SERIKALI YAKE


Rais John Magufuli amekamilisha kutengeneza muundo wa serikali yake na anatarajiwa kutangaza muundo huo katika Gazeti la Serikali (GN) muda wowote kuanzia sasa.Kutokana na kukamilika kwa muundo huo, Rais ameshatoa maelekezo ya utendaji kwa mawaziri wote na viongozi wengine kulingana na muundo wa serikali yake na hivyo wanatekeleza majukumu yao kutokana na maelekezo ya Rais.Hayo yalisemwa bungeni mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa anatoa majumuisho ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017.
Waziri Mkuu alisema baada ya kuapishwa, Rais alianza kazi ya kuunda serikali yake kwa kuteua mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine, kazi aliyoendelea kuifanya hadi hivi Aprili 20, mwaka huu alipoikamilisha.Alisema tofauti na magazeti la kawaida, GN hutolewa baada ya kukamilika kujengwa kwa hoja juu ya suala husika na ndio maana isingekuwa vema kwa Rais kutoa tangazo hilo wakati akiendelea kuunda serikali yake.
Share:

0 comments:

Post a Comment