MAGUFULI AOMBWA KUCHOMA MENO YA TEMBO, KWA NINI?
Wanaharakati wa Okoa Tembo wa Tanzania wamemshauri Rais John Magufuli kuteketeza shehena ya meno ya tembo yaliyohifadhiwa ghalani ili kuepuka gharama za uhifadhi na ulinzi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kampeni hiyo, Shubert Mwarabu amesema, endapo meno hayo yatauzwa yatachochea ujangili kwani itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida.
"Taiwan na China ambao ni miongoni mwa wateja wakubwa wa meno hayo wamefunga biashara hiyo kwenye masoko ya ndani hivyo haina sababu kutafuta wateja bali yachomwe," alisema.
Mwarabu amesema ili kuthibitisha kuwa biashara hiyo ni haramu, serikali haina budi kuonesha mfano wa wazi kwa kuteketeza meno hayo.
SOURCE
0 comments:
Post a Comment