Search This Blog

Wednesday, April 27, 2016

MBUNGE AHOJI MAJUKUMU YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU

Mwananchi's photo.
Mbunge Masoud Abdallah Salim leo amezua hali ya taharuki Bungeni pale alipokuwa akimuuliza waziri wa katiba na Sheria Dk Harison Mwakyembe kuhusu majukumu ya tume ya haki za Binadamu
Akiuliza swali la nyongeza Mbunge Salim amehoji kuhusu uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ikiwa ulikuwa huru na haki ikiwa ni pamoja na watu mbalimbali kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Aidha Mbunge huyo amehoji pia kuhusu baadhi ya wafungwa walio gerezani akielekeza shutuma dhidi ya mashekh wa jumuiya ya uamsho ambao hadi sasa wapo gerezani.
“Nataka kujua kuhusu lini mahabusu hawa kesi yao ya msingi itapatiwa ufumbuzi, kwani zipo taarifa kwamba wenzetu hawa wanafanyiwa vitendo vya ukatili gerezani.”Amesema Mbunge Masoud Abdallah Salim
Kufuatia hali hiyo Dk Mwakyembe amesema tayari wataalamu wa tume ya haki za binadamu inaandaa taarifa za utekelezaji wa haki za binadamu hivyo pindi taarifa hiyo itakapokamilika taarifa zitatolewa.
Share:

0 comments:

Post a Comment