Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka MSD kutoa maelezo kuhusu vifaa vya Sh. Bilioni 2 ambavyo 'viko njiani kwenda Muhimbili' kwa miaka 4.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu jana alisema bohari haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili bali imekuwa ikisambaza dawa zake nchi nzima
Katika ripoti ya CAG iliyotoka hivi karibuni, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema ukaguzi wao umebaini kuna dawa za thamani ya bilioni 2 zinaonekana zipo njiani toka Dsm Keko kwenda Hospitali ya Muhimbili Upanga tangu May mwaka 2012. Hazijafika Muhimbili hadi Leo - miaka 4!!
0 comments:
Post a Comment